1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 600 hawajulikani walipo North Carolina

1 Oktoba 2024

Wakaazi wa eneo la magharibi mwa jimbo la North Carolina nchini Marekani wanaendelea kuhesabu uharibifu uliotokea baada ya Kimbunga Helene kupiga katika eneo hilo.

Kimbunga Helene, North Carolina
Madhara ya Kimbunga Helene kwenye barabara za North Carolina.Picha: REUTERS

Zaidi ya watu 600 bado hawajulikani waliko kwa mujibu wa mshauri wa masuala ya usalama wa ndani wa Marekani, Liz Sherwood-Randall, aliyesema idadi hiyo inaweza kubadilika.

Zaidi ya watu 100 wamefariki katika nusu ya majimbo kufuatia kimbunga hicho kilichopiga eneo kubwa la Florida.

Soma zaidi: Biden kulitembelea jimbo la North Carolina

Wakaazi wameripotiwa kuedelea kukabiliwa na hali ngumu kufuatia barabara kufurika na ukosefu wa huduma za msingi kama umeme, maji na mawasiliano ya simu.

Athari za kimbunga hicho zimetatiza pia shughuli za kampeni za wagombea urais Kamala Harris na Donald Trump.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW