1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 7 wauawa katika mashambulizi Misikitini Nigeria

3 Septemba 2023

Watu waliojihami kwa silaha wamewaua waumini 7 wa dini ya Kiislamu na kuwajeruhi wengine watatu katika mashambulizi mawili tofauti katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Nigeria la Kaduna.

Askari wa usalama wakitoa ulinzi Nigeria baada ya moja ya matukio ya utekaji nyara
Askari wa usalama wakitoa ulinzi Nigeria baada ya moja ya matukio ya utekaji nyaraPicha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Msemaji wa polisi, Mansir Hassan amesema kuwa watuhumiwa wa magenge ya uhalifu walianza kurusha risasi Ijumaa kwa waumini katika jamii ya Saya-Saya wakati wa swala na kusababisha vifo vya watu sita.

Wahalifu hao tisa walifika eneo la tukio wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwashambulia watu Msikitini. Baadae walielekea kwenye kijiji jirani na kushambulia msikiti mwingine na kumuuwa mtu mmoja ambapo pia watu watatu walijeruhiwa.

Kaduna ni moja kati ya majimbo ya Kaskazini magharibi na kati mwa Nigeria ambayo yanakabiliwa na kitisho cha majambazi wanaovamia vijiji, kuua na kuteka nyara wakaazi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW