1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu 7 wauwawa kwa kombora kusini mwa Ukraine

30 Juni 2024

Makombora ya Urusi yalifyetuliwa katika mji wa kusini mwa Ukraine na kuua raia saba, wakiwemo watoto, na kujeruhi wengine 36.

Uharibifu ulioshuhudiwa baada ya mashambulizi ya makombora ya Urusi huko Vilniansk
Uharibifu ulioshuhudiwa baada ya mashambulizi ya makombora ya Urusi huko VilnianskPicha: Ukraine's President Volodymyr Zelenskiy via Telegram/via REUTERS

Wakithibitisha tukio hilo, mamlaka ya mji wa Vilniansk, ilichapisha picha ya miili ya watu ikiwa imefunikwa mablanketi na kutangaza siku moja ya maombolezo.

Gavana wa eneo hilo Ivan Fedorov amesema watoto watatu walikuwa miongoni mwa waliofariki na wengine tisa walijeruhiwa.

Katika taarifa tofauti iliyochapiswa kwenye mtandao wa Telegraph, Fedorov amesema shambulizi hilo liliharibu duka, majengo ya makazi na miundo mbinu muhimu katika mji huo wa Vilniansk, wenye idadi ya watu karibu 14,300 kabla ya uvamizi kamili wa Urusi mnamo Februari, 2022.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW