1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu 7 wauwawa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa India

8 Julai 2023

Watu 7 wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa leo nchini India baada ya kuzuka fujo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Bengal Magharibi linalofahamika kwa machafuko ya kisiasa wakati wa uchaguzi.

Indien | Wahlgewalt in Westbengalen
Picha: Satyajit Shaw/DW

Hayo yameelezwa na polisi ya jimbo hilo ambalo leo linafanya uchaguzi wenye ushindani mkali wa kuwapata viongozi wa manispaa. Zaidi ya wagombea 200, 000 wanawania nafasi hizo katika jimbo hilo lenye wakaazi milioni 104.

Mikanda ya video imeonesha wafanyakazi wa vyama hasimu wakizunguka mitaani wakiwa wamebeba bakora na masanduku ya kura waliyokwapua vituoni na katika maeneo mengine moto umewashwa nje ya vituo vya kupiga kura.

Soma zaidi:Uchaguzi wa India na Hofu za Jamii za Wachache 

Uhasama umeongezeka miaka ya karibuni baina ya wafuasi wa chama cha Trinamool Congress kinachotawala Jimbo la Bengal Magharibi  tangu mwaka 2011, dhidi ya wale wa chama cha waziri mkuu wa India Narendra Modi cha BJP kinachonuwia kujiongezea umaarufu kwenye jimbo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW