1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mafuriko yawauwa watu 8 Kenya, safari za ndege zavurugika

7 Machi 2026

Watu wanane wamefariki dunia katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumamosi. Juhudi za uokoaji zinaendelea.

Mafuriko ya Kitengengela, Kajiado 1.Mei 2024
Watu 8 wamefariki dunia kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini KenyaPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Licha ya juhudi hizo, Mkuu wa Polisi jijini Nairobi George Seda ametahadharisha kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Mvua kubwa zilianza kunyesha Ijumaa na kuendelea usiku kucha hali iliyosababisha magari kufunikwa na maji. Kiwango hicho kikubwa cha maji ya mvua pia kimeripotiwa kusababisha uharibifu kwa zaidi ya magari 100.

Safari za ndege zaathiriwa

Kutokana na mafuriko hayo, Safari za Shirika la Ndege la Kenya Airways zimevurugika na huenda hali hiyo ikaendelea kwa muda mrefu zaidi. Jeshi nchini humo limepelekwa kusaidia shughuli ua uokoaji ili kuwafikia wakaazi waliokwama katika maeneo mbalimbali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW