1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Watu 8 wauawa katika shambulizi la Urusi Kramatorsk

28 Juni 2023

Watu nane wameuawa katika shambulio la kombora la Urusi lililoupiga mgahawa maarufu katika mji wa mashariki mwa Ukraine wa Kramatorsk jana jioni.

Ukraine Krieg Angriff auf Kramatorsk
Wakaazi wa Kramatorsk wakiwa nje ya jengo lililoshambuliwa na makombora ya Urusi.Picha: Narciso Contreras/AA/picture alliance

Watu wengine wasiopungua 56 walijeruhiwa katika shambulio hilo lililoulenga mgahawa huo unaotembelewa zaidi na waandishi habari, wafanyakazi wa misaada na wanajeshi wanaoutumia mji wa Kramatorsk kama kituo cha operesheni zao.

Watoto watatu ni miongoni mwa waliokufa.

Mwendesha mashtaka mkuu Andrii Kostin amesema shambulio hilo lilitokea baada ya watu kurejea kutoka kazini.

Amesema watoto watatu waliokufa walikuwa na umri wa miaka 14 na 17.

Ukraine ilianzisha operesheni yake ya kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na Urusi mapema mwezi huu, ambayo mpaka sasa imepata mafanikio madogo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alitangaza Jumanne kuwa vikosi vya Ukraine vimesonga mbele katika kila upande.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW