1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu 80 wamekufa baada ya boti kuzama mtoni nchini Kongo

13 Juni 2024

Zaidi ya watu 80 wamekufa katika ajali ya boti iliyotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hayo yametangazwa na ikulu ya nchi hiyo jioni ya jana Jumatano.

Boti nchini Kongo
Boti nchini Kongo hujaza mizigo na abiria kupindukia uwezo.Picha: Junior Kannah/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo ya rais, boti iliyobeba mamia ya watu ilizama kwenye mto Kwango unaokatisha katika jimbo la Mai-Ndombe. Rais Felix Tshisekedi amesema amefadhaishwa na mkasa huo na kuamuru uchunguzi ufanyike kubani chanzo cha ajali hiyo.

Duru kutoka nchini humo zinasema ajali hiyo ilihusisha boti mbili, moja ikiwa njiani kuelekea mjini mkuu Kinshasa. Boti hiyo ilipata hitilafu ya injini na ilizama baada ya kugongwa na boti nyingine.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara nchini Kongo kutokana na nyingi kupakia kupindukia uwezo, matengenezo duni na sheria dhaifu za kusimamia uendeshaji wa vyombo vya majini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW