1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 81 wapoteza maisha kufuatia mafuriko Kenya

23 Machi 2026

Mamlaka za Kenya zasema mvua inaoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya Kenya imesababisha athari kubwa na maafa

Maafa kutokana na mafuriko yaripotiwa katika maeneo kadhaa ya Kenya ikiwemo mji mkuu Nairobi mwezi March
Maafa kutokana na mafuriko yaripotiwa katika maeneo kadhaa ya Kenya ikiwemo mji mkuu Nairobi mwezi MarchPicha: Boniface Muthoni/SOPA Images/Sipa USA/picture alliance

Mamlaka nchini Kenya jana zimefahamisha kwamba mvua kubwa ambayo imekuwa ikiendelea kunyesha nchini humo na kuleta mafuriko imesababisha vifo vya takriban watu 81 ndani ya mwezi huu.

Mamlaka ya Kenya pia imesema mvua hizo zinaendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi hiyo huku kanda ya Magharibi ikiathirika vibaya zaidi ambako baadhi ya vijiji vimezamishwa kabisa katika kaunti ya Kisumu na eneo la mashamba la hekari 1,200 likiharibiwa na mimeo kusombwa.

Watu 66 wapoteza maisha kutokana na mafuriko Kenya

Zaidi ya familia 3,000 zimelazimika kuyahama makaazi yao katika eneo la Nyakach,baadhi wakipata hifadhi kwenye vituo vinane vilivyowekwa kusadia waathika, wakati maji yanayomwagika kutoka mto Mirui yakiendelea kusababisha kitisho kwa jamii ya maeneo hayo.

Mamlaka pia zimesema mji mkuu Nairobi ndio ulioshuhudia vifo vingi vya watu 37 kufuatia mafuriko.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW