1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Watu 82 wauawa katika siku tatu za ghasia za kidini Pakistan

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Takriban watu 82 wameuwawa na wengine 156 kujeruhiwa kufuatia siku tatu za mapigano makali ya madhehebu ya kidini kaskazini-magharibi mwa Pakistan.

Pakistan religiös motivierte Unruhen in Kurram
Picha: Dilawer Khan/AFP/Getty Images

Pakistan ni nchi yenye Wasunni wengi lakini wilaya ya Kurram, karibu na mpaka na Afghanistan,  ina idadi kubwa ya Washia na jumuiya hizo zimepigana kwa miongo kadhaa.

Vurugu za hivi sasa zilianza siku ya Alhamisi wakati misafara miwili tofauti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wakisafiri chini ya ulinzi wa polisi ilipovamiwa, na kuua watu wasiopungua 43.

Mamlaka ya eneo hilo imeahidi kutafuta suluhisho la usitishaji mapigano kabla ya kushughulikia masuala ya msingi baina ya jamii hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW