Watu 85 wauwawa kufuatia mapigano makali Sudan
22 Mei 2024![Mwanawake na mtoto akikimbia vita Ukraine](https://static.dw.com/image/69041867_800.webp)
Matangazo
Mkuu wa mpango wa dharura wa shirika hilo Claire Nicolet, amesema siku ya Jumatatu pekee majeruhi tisa kati ya 60 waliopokewa katika hospitali ya kusini ya El-Fasher, walikufa kutokana na majeraha waliyoyapata.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja, mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya jeshi la serikali chini ya Abdel Fattah al-Burhan, na wanamgambo wa RSF wanaoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo.
El-Fasher ni mji mkuu pekee katika mkoa wa Darfur, ambaohaukochini ya udhibiti wa RSF na ni kitovu cha misaada ya kiutu katika kanda hiyo iliyo kwenye ukingo wa njaa.