1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Hekta 2,000 zateketea kwa moto Uhispania

3 Novemba 2023

Watu wapatao 850 wamehamishwa Ijumaa kutoka miji minne huku hekta takriban 2,000 za ardhi zikiteketea kutokana na moto wa msituni mashariki mwa Uhispania.

Takriban kekta 2,000 za ardhi za msituni mashariki mwa Uhispania zimeteketea moto.
Takriban kekta 2,000 za ardhi za msituni mashariki mwa Uhispania zimeteketea moto.Picha: Andreu Esteban/Europa Press/abaca/picture alliance

Wazima moto wapatao 200 na wanajeshi wa kitengo cha dharura wametumwa katika mji wa mashariki wa Montitxelvo katika mkoa wa Valencia ili kujaribu kuuzima moto huo.

Hayo yanajiri wakati eneo la Ulaya Magharibi likikabiliwa na dhoruba kali lililopewa jina "Ciaran" ambalo hadi sasa imesababisha vifo vya watu wasiopungua 10 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. 

Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa na Italia zilishuhudia upepo mkali, mafuriko, kukatika kwa umeme huku huduma za usafiri zikisitishwa kwa muda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW