1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 9 wajeruhiwa katika makombora ya Urusi mjini Dnipro

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Makombora ya Urusi yamelipiga jengo la makaazi ya raia na jengo jingine la karibu na idara ya usalama ya Ukraine katikati mwa jiji la Dnipro, kujeruhi watu 9 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Ukraine  Dnipro
Jengo lililolengwa na makombora ya Urusi huko DniproPicha: Hector Adolfo Quintanar Perez/picture alliance

Makombora ya Urusi yamelipiga jengo la makaazi ya raia na jengo jingine la karibu na idara ya usalama ya Ukraine katikati mwa jiji la Dnipro, kujeruhi watu 9 na kusababisha uharibifu mkubwa. Idadi ya waliuwawa kwenye mashambulizi ya Urusi yaongezeka

Meya wa mji wa Dnipro Borys Filatov alisema kuwa, hii ni mara ya tatu kwa jengo la idara ya usalama ya Ukraine SBU kulengwa katika mashambulizi ya Urusi. Shambulizi hilo, limesababisha Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy kuitisha mikutano ya dharura na idara ya usalama ya SBU, wizara ya mambo ya ndani, huduma za dharura na maafisa wa eneo hilo.

Vikosi vya Urusi vimezidisha mashambulizi ya makombora nyakati za usiku, vikilenga miundombinu kadhaa ikiwemo mji wa bandari wa Odesa, baada ya Moscow kujiondoa kwenye makubaliano ya usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW