1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 9 wauawa katika mapigano, Darfur

29 Desemba 2022

Watu tisa wameuawa kwenye mapigano katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan kati ya makundi ya Waarabu wa Rizeigat na watu wa Fur.

Sudan | Sicherheitskräfte nahe al-Geneina
Picha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Mashuhuda wamesema ufyatuaji risasi ulianza jana usiku katika eneo la Zalingei, mji mkuu wa Darfur ya Kati, baada ya mtu wa jamii ya Fur kuuawa na kuzusha mapigano makubwa. Msemaji wa shirika huru la misaada la Uratibu wa Wakimbizi Waliopoteza makaazi Adam Regal amesema watu waliokuwa na bunduki kutoka jamii ya Rizeigat waliwasili kwenye pikipiki katika kambi ya wakimbizi wa ndani mjini humo na kuwashambulia wakaazi wa Fur. Mapigano hayo yaliendelea usiku kucha hadi mapema leo. Machafuko ya kikabila hutokea mara kwa mara jimboni Darfur tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 2003. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu 300,000 wameuawa na milioni 2.5 wameachwa bila makaazi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW