1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Watu 9 wauawa kwa maandamano ya kupinga hukumu ya Sonko

2 Juni 2023

Watu tisa wameuawa katika mapigano yaliyozuka baada ya kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.

Senegal Unruhen nach Urteil gegen Sonko
Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Senegal, Antoine Diom amesema pamoja na vifo hivyo waandamanaji wameharibu mali za umma na na binafsi katika miji ya Dakar na Ziguinchor.

Mahakama ya Senegal ilimuondolea hatia ya ubakaji Sonko, lakini ikampatia adhabu ya kifungo cha miaka miwili kwa kuwapotosha vijana.

Katika siku za hivi karibuni Senegal imekuwa ikikabiliwa na vurugu za maandamano zilizosababisha na wafuwasi wanaolalamika kuwa changamoto hizo za kisheria dhidi ya Sonko zina lengo la kumweka kando ya ushiriki ya kinyang'anyiro cha urais.