1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wengi wahukumiwa kifungo Ubelgiji kwa biashara ya mihadarati

29 Oktoba 2024

Mahakama ya nchini Ubelgiji imewahukumu watu kadhaa adhabu ya vifungo jela, baada ya kufanyika kesi kubwa kuhusu dawa za kulevya nchini humo.

Mihadarati
Wengi wahukumiwa kifungo Ubelgiji kwa biashara ya mihadaratiPicha: Manish Kumar/DW

Vinara wa biashara hiyo wamepewa adhabu ya hadi miaka 17 jela. Washtakiwa zaidi ya 120 kutoka Ubelgiji, Albania, Colombia na Afrika Kaskazini walifikishwa mahakamani kwa kushiriki katika biashara ya kimataifa ya Cocaine na bangi baada ya wapelelezi kung’amua mawasiliano yao kwenye mitandao.

Kesi hiyo iliionesha uhusika wa Ubelgiji kama lango la Ulaya la kupitishia dawa za kulevya. Miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 17 jela, ni mwananchi wa Algeria. Waendesha mashtaka walitaka watu hao wapewe vifungo vya hadi miaka 20 jela.

Wamesema dawa za kulevya zinasafirishwa katika makontena kutoka Amerika ya Kusini na Morocco na kuletwa kwenye bandari za Ubelgiji, Uholanzi, Ujerumani na Ufaransa kabla ya kuuzwa barani Ulaya kote. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW