1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lori lagonga kituo cha basi mjini Tel Aviv na kujeruhi kadha

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Watu kadhaa wamejeruhiwa nchini Israel baada ya lori kugonga kituo cha basi, kaskazini mwa mji wa kibiashara wa Tel Aviv leo Jumapili.

Ajali ya lori mjini Tel Aviv
Ajali ya lori mjini Tel AvivPicha: Jack Guez/AFP

Watu kadhaa wamejeruhiwa nchini Israel baada ya lori kugonga kituo cha basi, kaskazini mwa mji wa kibiashara wa Tel Aviv leo Jumapili.

Polisi hawakusema kwa haraka chanzo cha ajali hiyo au ikiwa ni shambulio. Kulingana na huduma ya dharura, watu 16 wamekimbizwa hospitali za karibu na polisi pia wamethibitisha majeruhi kadhaa.

Wakati huo huo madkatari wa Palestina wamesema shambulizi la anga la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, limewaua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine mapema leo asubuhi, wakati vikosi vya Israel vikizidisha kampeni yake kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Israel yauwa 28 Gaza, 3 Lebanon

Madaktari hao wameongeza kuwa shambulizi hilo jipya limeharibu nyumba kadha huko Jabalia, kambi kubwa zaidi kati nane za kihistoria za Ukanda wa Gaza, ambayo imekuwa kiini cha kampeni za kijeshi za Israel kwa zaidi ya wiki tatu.