Watu kadhaa wakufa Kongo katika mlipuko wa lori ya mafuta
15 Septemba 2022Matangazo
Gavana wa mkoa wa Kongo Central Guiy Bandu ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa mlipuko huo ulitokea usiku wa kuamkia Alhamisi katika kijiji cha Mbuba, karibu kilometa 120 magharibi mwa mji mkuu Kinshasa.
Zaidi ya watu 50 waliuawa katika mlipuko wa lori la kusafirisha mafuta katika kijiji hicho Oktoba mwaka wa 2018.
Kijiji cha Mbuba kipo kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi inayouunganisha mji mkuu Kinshasa na bandari za Matadi na Boma.
Gavana Bandu amesema wakati umefika sasa wa kuchukua hatua kali za kuimarisha sheria za usafirishaji, hasa wa bidhaa zinazoweza kuwaka moto kwa haraka, ili kukomesha kujirudia kwa ajali za aina hiyo.