1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yasababisha vifo, watu kukosa makazi Ulaya ya Kati

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Watu wawili wamekufa Poland na Austria kutokana na mvua kubwa zinazoendelea Ulaya ya kati. Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amethibitisha kifo cha mwanamume kilichotokea mmoja karibu na mji wa Kodzko.

Mafuriko Ulaya ya kati
Sehemu ya hali inavyoonekana kutokana na mvua kubwa PolandPicha: Krzysztof Zatycki/IMAGO/ZUMA Press Wire

Takriban watu 1,600 wamehamishwa kutoka eneo hilo na mamlaka za Poland zimeomba msaada wa jeshi kusaidia uokoaji.Mtu aliyekufa kutokana namvua hizo Kaskazini mashariki mwa Austria ni mwanamume  aliyekuwa mfanyakazi wa idara ya zimamoto.

Soma zaidi: Ulaya ya Kati yakumbwa na mafuriko

Huko Jamhuri ya Czech, polisi wamesema, watu watatu waliokuwa kwenye gari lililozolewa na maji na kutumbukia kwenye mto katika mji wa Lipova Lazne hawajulikani walipo. Mwanamume mwingine ametoweka baada ya kusombwa na mafuriko eneo la kusini mashariki.

Nako Kusini mashariki mwa Romania, watu wanne wamekufa na miili yao imepatikana katika eneo lililoathiriwa vibaya zaidi na mafuriko la Galati. Takriban nyumba 5,000 zimeharibiwa kutokana na mvua hizo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW