1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa Ukraine

10 Juni 2023

Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mji wa bandari wa Odessa nchini Ukraine wakati wa mashambulio ya usiku ya ndege zisizokuwa na rubani. Haya yamesemwa leo na jeshi la Ukraine.

Ukraine | Zerstörung nach russischen Dronenangriffen in Odessa
Picha: UKRAINIAN ARMED FORCES/REUTERS

Kupitia mtandao wa Facebook, kamandi ya kijeshi ya Kusini mwa Ukraine imeandika kuwa vifusi kutoka kwa ndege isiyo na rubani ya Urusi iliyodunguliwa na jeshi la anga la Ukraine, vilianguka ndani ya jengo la ghorofa nyingi na kuwaka moto. Raia watatu waliuawa katika moto huo na wengine 26 kujeruhiwa.

Ndege 20 zisizokuwa na rubani za Iran zadunguliwa

Wakati huohuo,  jeshi la anga la Ukraine limesema kuwa Urusi imeelekeza ndege 35 zisizokuwa na rubani na makombora manane katika malengo nchini Ukraine. Jeshi hilo limeongeza kuwa ndege 20 za Iran zisizokuwa na rubani aina ya Shaheed zilidunguliwa pamoja na makombora mawili.

Jeshi hilo limeendelea kusema kuwa mbali na Odessa, mashambulizi hayo ya Urusi pia yalikuwa yameelekezwa dhidi ya malengo katika maeneo ya Poltava na Kharkiv.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW