1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Watu kadhaa waokolewa, miili yatolewa mgodini Afrika Kusini

14 Januari 2025

Zaidi ya wachimba migodi haramu 26 wameokolewa na karibu miili kumi kuondolewa kwenye mgodi uliotelekezwa nchini Afrika Kusini.

Operesheni za uokozi zilianza tena leo kuwafikia watu zaidi ambao huenda bado wamekwama mgodini humo. Kiongozi wa jamii ya eneo hilo, Johannes Qankase, amesema wachimba migodi waliookolewa ni wamedhoofika mno na wana upungufu wa maji mwilini.

Amesema wengi wao wamepelekwa hospitali wakati wawili wanaaminika kuwekwa kizuizini na polisi. Maafisa wa serikali wanatarajiwa kulitembelea leo eneo hilo la mgodi huku shughuli ya uokozi ikiendelea.

Soma pia: Ramaphosa: Maisha ya wachimba migodi hayapaswi kuhatarishwa

Operesheni hiyo inafuatia sakata ya wiki kadhaa kwenye mgodi huo uliotekelezwa, ambapo maafisa wanatuhumiwa kwa kujaribu kuwalazimisha wachimbaji hao kujitokeza nje kwa kuzuia chakula na maji kuteremshwa kwao na jamii ya eneo hilo.

Haijulikani wazi ni watu wangapi waliobaki kwenye mgodi huo. Serikali imesema jana kuwa zaidi ya watu 1,000 wanaohusika na uchimbaji haramu wa madini katika eneo hilo wametoka mgodini na kukamatwa mpaka sasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW