1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu kumi wameuwawa Ethiopia kufuatia maporomoko ya udongo.

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Watu kumi wameuwawa katika maporomoko ya udongo kwenye jimbo la Amhara Ethiopia. Shirika la habari la Amhara limeripoti likimnukuu msimamizi wa eneo hilo Tesfaye Workneh akisema miili minne iliopolewa kwenye matope.

Amhara, Ethiopia | maporomoko ya udongo Gondar
Maporomoko ya udongo katika eneo la Gondar kwenye jimbo la Amhara EthiopiaPicha: North Gondar zone Disaster Prevention department

Shirika hilo limemnukuu afisa huyo akisema watu wengine wanne walijeruhiwa vibaya na wanaendelea na matibabu, na kuongeza kwamba takriban watu 2,400 wameyahama makaazi yao kufuatia mkasa huo na kwa sasa wanahifadhiwa na taasisi mbalimbali za kijamii.

Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa ikinukuu mamlaka ya hali ya hewa Ethiopia ikionya juu ya hatari kubwa ya mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi katika maeneo mengi ya taifa hilo la pembe ya Afrika. 

Soma pia:Mafuriko, maporomoko yaua watu 75 nchini Brazil

Maporomoko ya ardhi ya hivi karibuni nchini humo yalisababisha vifo vya watu 229 huku wengine maelfu wakiyahama makaazi yao huko Kencho Shacha Gozdi kusini mwa Ethiopia mwezi Julai.