1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Watu 10 wauawa katika mji wa mpakani wa Urusi wa Belgorod

30 Desemba 2023

Maafisa wa Urusi wamevishutumu vikosi vya Ukraine kwa kuushambulia kwa makombora mji wa mpakani wa Belgorod na kusababisha vifo vya watu 10 wakiwemo watoto watatu.

Ukraine-Krieg Belgorod Novaya Tavolzhanka | Beschuss durch Russland
Raia wa Urusi akishuhudia nyumba yake iliyoharibiwa na shambulio la Ukraine katika mji wa mpakani wa Belgorod:04.07.2023Picha: AFP

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na Gavana wa mkoa huo wa Belgorod, Vyacheslav Gladkov.

Hayo yanajiri siku moja baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa kote nchini Ukraine na kuuwa takriban raia 39. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hii leo kuwa shughuli zinaendelea sehemu mbalimbali ili kurejesha hali ya kawaida baada ya mashambulizi hayo.

 Urusi na Ukraine zimedai hata hivyo kuzima mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani katika maeneo mbalimbali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW