Watu masikini waathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi
14 Novemba 2016Takribani watu milion 26 wanatumbukia katika umasikini mkubwa kila mwaka jambo ambalo linarudisha nyuma matumizi ya kimataifa ya huduma na bidhaa mpaka wastani wa bilion 520 kwa mwaka. Wakati huo huo umoja wa mataifa umeonya kuwa kunaweza kuwa na majanga zaidi ikiwa hakutakuwa na udhibiti wa ongezeko la joto duniani.
Katika utafiti mpya wa benki hiyo inaelezwa kwamba majanga ambayo husababishwa na hali mbaya ya hewa pamoja na matetemeko ya ardhi, yamekuwa yakipuuzwa kwa hadi asilimia 60 kwa sababu ya hali za watu masikini kupuuzwa, na hivyo kusababisha madhara kwa watu na vilevile katika uchumi.
Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim katika taarifa yake amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia kurudisha nyuma juhudi za miongo kadhaa za kupambana na umasikini, wakati Arin de Hoog kutoka shirika linalijishughilisha na mazingira akisema kuwa, kinachokosekana sasa ni vuguvugu halisi kutoka kwa viongozi wa dunia katika kuchukua hatua za kutunza nishati asilia.
Miaka ya hivi karibuni yavunja rekodi kwa kuwa na joto zaidi
Kiwango cha wastani cha joto kwa mwaka huu kilitarajiwa kufikia nyuzi joto 1.2, zaidi ya viwango vya kabla ya mageuzi ya viwanda ikiwa na maana kwamba miaka 16 kati ya 17 yenye joto zaidi imerekodiwa katika karne hii, hii ni kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa duniani WMO.
Rekodi hii mpya ina maana kwamba ulimwengu uko katika hatari zaidi ya nusu ya ukomo wa juu wa nyuzi joto 2 wa hali jumla ya ongezeko la joto, ikiwezekana nyuzi joto 1.5 ambayo mataifa wanachama wa umoja wa mataifa walikubaliana ili kudhibiti athari mbaya kabisa za mabadiliko ya tabia nchi
Hali ya hewa iliyosababisha elnino ilipunguza joto katika miezi ya mapema ya mwaka, lakini hata baada ya athari zake kuonekana kupungua kiwango cha joto kilibaki juu.
Ripoti hiyo inakariri kuwa mafuriko na tetemeko la ardhi yanaweza kuwa hatari zaidi kwa watu masikini, madhara yanaonekana kutokuwa na madhara katika uzalishaji wa uchumi wa nchi kwa huwa huwaathiri watu ambao hawamiliki vitu na wenye kipato cha chini.
Lengo la ripoti hiyo ni kuzisaidia nchi kuchochea mjadala wa kisera ili kuweza kuthibiti madhara, pia kuzisaidia nchi kutengezea muongozo wa mipango yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwasilisha katika makubaliano ya Paris ambayo yameanza kufanya kazi Novemba 4.
Mwandishi. Celina Mwakabwale/AFP/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu