1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Watu nane wauawa kwa shambulio nchini mali

5 Januari 2025

Duru zimeripoti mapema leo kwamba takriban watu wanane wameuawa katikati mwa Mali huku jeshi la nchi hiyo na kundi la mamluki la Kirusi la Wagner wakishutumiwa kwa shambulio hilo.

Mali Bamako  I Assimi Goita
Mtawala wa kijeshi wa Mali Assimi GoitaPicha: AP Photo/picture alliance

Duru zimeripoti mapema leo kwamba takriban watu wanane wameuawa katikati mwa Mali huku jeshi la nchi hiyo na kundi la mamluki la Kirusi la Wagner wakishutumiwa kwa shambulio hilo la hivi karibuni katika nchi hiyo yenye machafuko ya Afrika Magharibi.

Afisa wa eneo hilo amelimbia shirika la habari la AFP kwamba gari aina ya Hilux iliyokuwa inaelekea katika kambi ya wakimbizi nchini Mauritania ilishambuliwa kwa risasi na wanajeshi wa Mali na wale wa kundi la Wagner na kuwauwa watu hao siku ya Alhamisi.

Soma zaidi. Mali: Tumemkata kiongozi wa tawi la IS Sahel

Jeshi la Mali halijatoa tamko lolote juu ya shutuma hizo. Mali imegubikwa na machafuko makubwa tangu mwaka 2012 yanayohusishwa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu IS pamoja na magenge ya wahalifu katika eneo hilo.

Na hivi karibuni watawala wa kijeshi wa nchi hiyo walivunja uhusiano na mkoloni wa zamani Ufaransa na kuanzisha uhusiano wa kijeshi na kisiasa na Urusi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW