1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Watu nusu milioni Crimea hawana huduma ya umeme

27 Novemba 2023

Takriban watu nusu milioni katika jimbo la Crimea hawana huduma ya umeme kuufuatia kimbunga kibaya.

Ukraine | waokoaji wakitumia tochi kuendelea na uokoaji
Waokoaji wakiokoa manusura baada ya dhoruba kupiga CrimeaPicha: Governor Mikhail Razvozhayev/AP/picture alliance

Takriban watu nusu milioni wameachwa bila huduma ya umeme baada ya kimbunga kilichopiga katika eneo labahari nyeusi kusababisha mafuriko yaliyozifunika barabara,na kung'oa miti pamoja na kuharibu nyaya za umeme katika jimbo la Crimea.

Shirika la habari la serikali laUrusi limesema kwamba mtu mmoja pia amepoteza maisha kufuatia kimbunga hicho´ambacho kilipiga pia Kusini mwa nchi hiyo na kusababisha wimbi kubwa la mafuriko yaliyofika hadi mji wa kitalii wa Sochi na kusababisha uharibifu,ikiwemo nyumba na shule kuharibiwa.

Soma pia:Kyiv yadai kuishambulia kambi ya Urusi huko Crimea

Kimbunga hicho ni sehemu ya hali mbaya ya hewa iliyosababisha ukosefu wa umeme katika maeneo mengi kutokana na theluji nyingi iliyoanguka na upepo mkali katika nchi za Romania na Moldova jana jumapili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW