1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wafa katika ajali ya gari kusini mwa Ujerumani

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Ajali hiyo imetokea karibu na Muehldorf, mashariki mwa mji wa Munich katika barabara ya A94 inayomalizikia katika mpaka wa Austria.

Schweden Lars Vilks
Picha: Johan Nilsson/TT/IMAGO

Watu saba wamekufa katika ajali kusini mwa Ujerumani wakati gari lililokuwa likijaribu kukwepa upekuzi wa polisi lilipoacha barabara kuu likiendeshwa kwa kasi kubwa na kupinduka.

Maafisa wanasema gari hilo lilikuwa limejaza watu na lilionekana lilikuwa limewabeba wahamiaji. Ajali hiyo imetokea karibu na Muehldorf, mashariki mwa mji wa Munich katika barabara ya A94 inayomalizikia katika mpaka wa Austria.

Polisi imesema uchunguzi wa awali unaonesha lilikuwa ni gari lililotumiwa kuwabeba wahamiaji kwa njia isiyo halali, likiwa na watu zaidi ya 20. Polisi wamesema waendesha mashitaka wamefungua uchunguzi wa mauaji.

Shirika la habari la Ujerumani dpa limeripoti kwamba wahamiaji wengine wote wakiwemo watoto, wamepata majeraha madogo madogo na wengine makubwa na wamepelekwa katika hospitali zilizo karibu. Haikufahamika mara moja walikotokea wahamiaji hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW