1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wafa kwenye maporomoko ya udongo Uganda

26 Mei 2023

Watu saba wa familia moja wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo mashariki mwa Uganda kufuatia maporomoko ya tope yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha wilaya ya Bulambuli.

Uganda | Erdrutsch
Picha: Uganda Red Cross Society/AP Photo/picture alliance

Kulingana na mkuu wa wilaya hiyo Stanley Bayola mvua hiyo iliyoandamana na upepo mkali ilinyesha  kwa muda wa saa saba na kusababisha uharibifu mkubwa kwa makazi  na mashamba ya watu wa eneo hilo.

Juhudi za kufukua maiti za wahanga na pia kuwanusuru baadhi ya watu waliokwama katika vifusi zinaendelea kwa  sasa.

Maporomoko yaua watu 34 Uganda

Inahofiwa kuwa idadi ya waliopoteza maisha yao inaweza kuongezeka kutokana na mazingira magumu ya kuwafikia watu wa familia kadhaa ambazo njia yao ya kujinusuru inazidi kuwa ngumu.

Visa kama hivyo vya maporokomo ya ardhi na tope hutokea mara kwa mara eneo hilo na watu hushauriwa kuchukua tahadhari katika msimu wa mvua. Ila kwa wengi ni vigumu kwao kuyahama makazi yao ya muda mrefu.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW