Watu saba wakamatwa Ujerumani wakihusishwa na "IS"
31 Mei 2023Matangazo
Wakati huo huo, polisi wamefanya misako 19 katika majimbo ya Baden-Wuerttemberg, Bremen, Hamburg, Hesse, North Rhine-Westphalia na Rhineland-Palatinate, pamoja na eneo moja nchini Uholanzi. Washukiwa hao wamekamatwa kwa tuhuma za kukusanya michango na kuipeleka kwa IS. Waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa leo na kesho mbele ya mahakama kuangalia iwapo wanapaswa kubakia kizuizini kabla ya kesi yao kusikilizwa. Fedha hizo zilikusanywa kupitia kampeni za kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na majina kama vile ''Dada Yako Kambini,'' ambazo zimekuwa zikiendeshwa kwa miaka kadhaa.