1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wamekufa kwa ajali ya boti Kenya

23 Septemba 2021

Afisa moja nchini Kenya amesema watu saba wamekufa baada ya boti yao kuzama katika ziwa Victoria.

Videostills eco@africa Wasserhyazinthe
Picha: DW

Kamishna wa kaunti ya Homa Bay Moses Lilan, amesema miili saba imeopolewa kutoka ziwa Victoria baada ya ajali iliyotokea siku ya Jumanne, ukiwepo wa mtoto. Maafisa wanasema watu wanne bado hawajapatikana.

Polisi imesema abiria 19 walikuwa kwenye boti wakati ilipozama ikiwa umbali wa chini ya nusu kilomita kutoka kituo cha maegesho.

Kamishna wa Kaunti hiyo anasema boti hiyo ilikuwa imejazwa abiria na mizigo kupita kiasi.

Lakini Felix Ouma, aliekuwa anaendesha boti hiyo, alisema hali mbaya ya hewa na gugu maji ndiyo vilisababisha ajali hiyo.

Ajali kama hizo hutokea mara kwa mara kwenye ziwa hilo na hugharimu maisha ya makumi kadhaa ya watu kila mwaka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW