1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wauawa katika machafuko Iran:

22 Februari 2004

TEHERAN: Nchini Iran wameuawa si chini ya watu saba katika machafuko yaliyotokea baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa bunge. Shirika la Habari la Wanafunzi ISNA liliarifu kuuawa watu wanne katika mapigano ya njiani katika jimbo la uchaguzi Iseh, wapiga kura waliovunjwa moyo walipojaribu kulishambulia jengo la polisi. Mjini Firusabad jimboni Fars polisi waliwapiga risasi na kuwauawa wafanya maandamano watatu wanaosemekana walilalamika dhidi ya kiini macho cha kura, aliripoti mwanasiasa mmoja. Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kuwa asili miya 51 ya wapiga kura walishiriki katika uchaguzi. Kiwango hicho ni cha chini kabisa tangu miaka 25. Gazeti la mrengo wa kiasilia "Jam e Jam" limeripoti kuwa wagombea wa kiasilia wamenyakua viti 108 kutoka jumla ya viti 157, ikiwa na maana kuwa wafuasi waa mrengo wastani wamenyakua viti 25 tu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW