1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wauawa katika machafuko Uganda

16 Januari 2026

Takribani watu saba wameuwawa katika machafuko usiku wa kuamkia leo katikati mwa Uganda, siku moja baada ya uchaguzi wa kitaifa ambao unaonekana kumrejesha madarakani Rais Yoweri Museveni kwa muhula mwingine.

Uganda Kampala 2026
Polisi ya Uganda ikipiga doria katika mjini Kampala baada ya uchaguzi.Picha: Rian Cope/AFP/Getty Images

Ghasia zimeripotiwa katika maeneo ya Butambala, ambako polisi na mbunge wa eneo hilo walitoa maelezo yanayokinzana kuhusu chanzo cha vifo hivyo.

Polisi walisema kundi la wafuasi wa upinzani lilishambulia kituo cha polisi, huku mbunge Muwanga Kivumbi akidai kuwa watu waliuawa ndani ya nyumba yake walipokuwa wakisubiri matokeo ya uchaguzi wake.

Matokeo ya awali yanaonyesha Museveni anaongoza kwa zaidi ya asilimia 75, huku mpinzani wake Bobi Wine akidai udanganyifu mkubwa na kutangaza kuwa vikosi vya usalama vilikuwa vimezingira nyumba yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW