1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaRwanda

Watu sita wafariki dunia Rwanda kufuatia mripuko wa Marburg

30 Septemba 2024

Watu sita wameripotiwa kufariki dunia nchini Rwanda kufuatia mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg (MVD) nchini Rwanda.

Afisa wa afya nchini Ivory Coast akitayarisha chanjo dhidi ya virusi vya Ebola huko Cocody mnamo Agosti 16, 2021
Afisa wa afya nchini Ivory Coast akitayarisha chanjo dhidi ya virusi vya EbolaPicha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, waziri wa afya nchini humo Sabin Nsanzimana, amesema jumla ya watu  26 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo wa ambao awali ulijulikana kama homa ya Marburg (MHF) .

Nsanzimana amesema hadi kufikia sasa, watu 20 wamethibitishwa kupata maambukizi ya ugonjwa huo huku wengine sita wakifariki dunia.

Soma pia:Tanzania yatangaza kudhibitiwa kwa homa hatari ya Marburg

Kwasasa, wagonjwa 20 wanaotibiwa ,  zaidi ni wahudumu wa afya  na wametengwa huku uchunguzi kuhusu chanzo cha mripuko huo ukiendelea.

Hatua za kinga pia zimeimarishwa katika vituo vyote vya afya.

Dalili za ugonjwa wa homa ya Marburg MVD ni pamoja na kuumwa na tumbo, kutapika damu na kuharisha. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni takriban asilimia 88 ya wale walioambukizwa ugonjwa huo, hufariki dunia.

Afisa wa afya wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Umma akivalia mavazi ya kinga dhidi ya virusi vya Ebola akinyunyiza dawa katika kituo cha afya huko Cocody Picha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Virusi vya ugonjwa huo vimepewa jina hilo la mji wa Ujerumani Marburg kwasababu msaadizi mmoja wa maabara mjini humo, aliambukizwa ugonjwa huo ambao bado ulikuwa haujajulikana mnamo mwaka 1967 alipokuwa akimshughulikia tumbili aliyekuwa ameambukizwa.

Nchi jirani ya Tanzania ilikuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo mnamo mwaka 2023 huku Uganda ikipata maambukizi kama hayo mwaka 2017.

Soma pia:Watu watano wafariki Tanzania baada ya mripuko wa homa ya Marburg

Huku kukiwa na asilimia 88 ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, virusi vya Marburg, vinafananishwa na vile vya ugonjwa wa Ebola, na kuambukizwa watu kutoka kwa popo.

Baadaye huenea kwa binadamu kupitia maji maji ya mwili ya watu walioambukizwa.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW