1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina sita wauwawa Gaza

5 Januari 2024

Takriban watu sita wameuwawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israel katika eneo la mji wa Rafah huko mjini Gaza.

Gazastreifen Luftangriffe auf Khan Younis
Moshi ukifuka juu ya mji wa Khan Yunis kwa upande wa Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel Januari 2, 2024.Picha: AFP/Getty Images

Tukio hilo linatokea katika kipindi ambacho waziri wa mambo ya nje ya Marekani akiwa safarini kuelekea Mashariki ya Kati na wa Ujerumani akitarajiwa kuzuru eneo hilo Jumapili.

Maelfu ya Wapalestina wamejazana katika mji wa Rafah, mojawapo ya maeneo ambalo Israeli imewataka walifanye kuwa kimbilio lao la kiusalama, ingawa majeshi ya Israel yameonekana kuendelea kufanya mashambulizi katika sehemu zote za Ukanda uliozingirwa wa Gaza.  Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema maelfu kadhaa ya wapiganaji wa Hamas wamesalia kaskazini mwa Gaza, ambako vitongoji vyote vimeripuliwa na kuwa kifusi.

Mapigano makali pia yanaendelea katikati mwa Gaza na mji wa kusini wa Khan Younis, ambapo maafisa wa Israel wanasema muundo wa kijeshi wa Hamas bado upo madhubuti.

Baerbock anataka Israel iwalinde raia huko Gaza

Kabla ya kuanza safari yake ya Mashariki ya Kati, Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anasisitiza kuwa Israel lazima ifanye zaidi kwa ajili ya ulinzi wa raia katika vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza.

Waziri Baerbock akiwa katika mkutano wa chama chake cha Walinzi wa Mazingira huko Karlsruhe.Picha: Jens Thurau/DW

Aidha ametoa wito wa kusimamisha mapigano kwa ajili ya kutoa misaada ya kiutu, kwa kusema amani haiwezi kupatikana ikiwa matarajio ya maisha yenye hadhi yanaondoshwa, kama vile Gaza sio sehemu ambayo haitakalika baada ya vita."Lazima kusiwe na ukaliwaji kwa kimabavu katika Ukanda wa Gaza baada ya vita, Wapalestina wasifukuzwe na kusipunguzwa kwa ukubwa wa eneo hilo. Lakini vilevile kusiwe na hatari tena kwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza." alisema Baerbock.

Hiyo itakuwa ni ziara yake ya nne katika eneo hilo tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas katika ukanda wa Gaza na anatarajiwa kuafanya mazungumzo na waziri mambo ya nje wa Israel, Yisrael Katz pamoja na Rais Isaac Herzog, kadhalika atakutana na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas na waziri wa ke wa nje Riyad al-Maliki.

Lebabon yalalamika Israel kufanya mashambulizi katika ardhi yake.

Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa SALEH AL-AROURI aliyeuwawa katika mlipuko huko Beirut.Picha: APA Images/ picture alliance

Katika hatua nyingine Lebanon imewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia mauaji yaliyolengwa na Israel kwa Naibu mkuu wa Hamas Saleh al-Arouri katika mji mkuu Beirut kwa kusema hatua hiyo ni "awamu hatari zaidi" ya mashambulio ya Israeli dhidi ya taifa lao.

Malalamiko hayo yameandikwa tarehe 4, lakini Shirika la Habari la Uingereza Reuters limefanikiwa kuyaona hivi karibuni. Taarifa iliyomo inasema Israel ilitumia makombora sita katika shambulio hilo lililomuua Arouri na kuongeza kuwa Israel inatumia anga ya Lebanon kuishambulia Syria.

Soma zaidi:Israel yaainisha mkakati mpya wa mashambulizi Gaza

Uvamizi huu wa Israel katika Ukanda wa Gaza ulikuwa ni jibu kwa mashambulizi ya Hamas na makundi mengine nchini Israel ya Oktoba 7, ambapo watu 1,200, wakiwemo raia 800 waliouwawa, huku upande wa Hamas ukieleza idadi ya waliuwawa tangu wakati huo kufikia 22,438, wengi wao raia.

Chanzo: RTR

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW