1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu tisa, wakiwemo askari wanne, wameuawa Sudan

24 Julai 2023

Watu tisa, wakiwemo askari wanne, wameuawa jana usiku wakati ndege ya kiraia ilipoanguka nchini Sudan kutokana na sababu za kiufundi.

Egypt launches fresh Sudan mediation attempt at summit
Picha: Ibrahim Mohammed Ishak/REUTERS

Mapigano hayo yamesababisha mamilioni ya watu kunasa majumbani mwao na baadhi wakiwa bila ya maji, hasa katika viunga vya mji mkuu Khartoum ambako wakaazi wanatoa wito wa misaada ya chakula ili kuwasaidia kuishi.

Katika mji wa Port Sudan, pwani ya mashariki ambayo kwa kiasi kikubwa imenusurika vita hivyo mpaka sasa,jeshi limesema mtoto alinusurika ajali ya ndege aina ya Antonov ambayo iliwauwa watu wengine tisa.

Soma pia:Sudan yatimiza siku 100 za mapigano

Uwanja wa ndege wa Port Sudan ndio wa pekee unaondelea kufanya kazi nchini humo kutokana na mgogoro wa kivita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW