1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Watu tisa washtakiwa Rwanda kwa kueneza habari za uongo

19 Oktoba 2024

Serikali ya Rwanda imewafungulia watu tisa mashitaka ya usambazaji habari za uongo, ambayo adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 15 jela.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Lim Yaohui/Newscom/Singapore Press Holdings/IMAGO

Washukiwa hao walifikishwa katika mahakama kuu ya Kigali huko Nyamirambo hapo jana, ambako walisomewa mashitaka ya kueneza propaganda kwa nia ya kusababisha mtazamo mkali wa kimataifa dhidi ya serikali ya Rwanda.

Pia walishutumiwa kwa kujiunga na shirika la uhalifu na njama ya kufanya uhalifu dhidi ya uongozi wa nchi hiyo.

Upande wa mashtaka waomba hukumu kali dhidi ya washtakiwa

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama iwahukumu kifungo cha miaka 15 jela kwa washtakiwa saba na miaka 10 kwa wengine wawili.

Hakimu aamuru kikao kuendelezwa kwa faragha

Vyanzo kutoka mahakamani hapo vilisema wakati kesi ilipokuwa ikiendelea, hakimu wa mahakama hiyo aliamuru kuendelezwa faraghani na kuwaagiza waandishi wa habari, jamaa na baadhi ya wafuasi wa upinzani kutoka nje.

Kwa muda mrefu, upinzani wa kisiasa na uhuru wa kujieleza nchiniRwanda umekandamizwa chini ya utawala wa miongo mitatu wa Rais Paul Kagame.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW