1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu tisa wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

19 Novemba 2025

Watu tisa wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia shambulio la Urusi usiku wa kuamkia leo katika eneo la Ternopil magharibi mwa Ukraine.

Ternopil 2025 | Watu 9 wameuawa na wengine takriban 40 wamejeruhiwa
Jengo lililolengwa na mashambulizi ya Urusi huko Ternopil yaliyosababisha vifo Picha: State Emergency Service of Ukraine/Handout/Anadolu/IMAGO

Hayo yameelezwa hivi leo na Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky . Aidha kumeshuhudiwa pia mashambulizi mengine ya droni na makombora katika mji mwingine wa Lviv na kuilenga miundombinu ya nishati na kupelekea kaya kadhaa kukosa umeme.

Urusi imesema mashambulizi hayo ni ya kujibu kile ilichotaja kuwa "vitendo vya kigaidi vya Ukraine".

Nchi ya Poland ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya  NATO na inayopakana na eneo la magharibi mwa Ukraine, imelazimika kuvifunga kwa muda viwanja vya ndege vya Rzeszow na Lublin kusini mashariki mwa nchi hiyo na kuimarisha ulinzi wa anga lake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW