1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Lebanon: Milipuko katika 'pagers' yauwa 9 na kujeruhi maelfu

18 Septemba 2024

Watu wasiopungua tisa wameuawa na maelfu kujeruhiwa baada ya mamia ya vifaa vya mawasiliano kulipuka nchini Lebanon. Waziri wa Afya Firas Fabias amethibitisha idadi hiyo ya vifo, ambavyo miongoni mwake ni msichana.

Lebanon I milipuko ya Pagers
Majeruhi akipandishwa kwenye gari la wagonjwa kufuatia mkasa wa kulipuka vifaa vya mawasiliano, PagersPicha: Hussein Malla/AP/picture alliance

Amesema watu wasiopungua 2,750 wamejeruhiwa na zaidi ya 200 wana hali mbaya kwenye maeneo kadhaa ya Lebanon na hasa yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Hezbollah.

Kundi hilo limesema wapiganaji wake wawili pia wameuawa na wengine wamejeruhiwa nchini Syria ambako pia kumetokea milipuko.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kitisho cha kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na Hezbollah kufuatia kisa hicho kinachotokea katika mazingira tete na kuongeza hali ya wasiwasi.

Gazeti la Marekani la New York Times limeripoti baada ya mkasa huo kwamba vifaa hivyo vilitengenezwa Taiwan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW