JamiiAfghanistan
Watu 17 wafariki Afghanistan kufuatia mafuriko
29 Machi 2026
Matangazo
Kwa mujibu wa mamlaka, majimbo 13 miongoni mwa 34 ya nchi hiyo yameathirika, hasa maeneo ya magharibi, kati na kaskazini-magharibi mwa Afghanistan.
Zaidi ya nyumba 140 zimeharibiwa, kilomita zipatazo 80 za barabara zimesombwa na maji, huku mashamba na mifumo ya umwagiliaji pia vikiharibiwa.
Zaidi ya kaya 500 zimeathirika. Mamlaka zimesema, idadi ya vifo inaweza kuongezeka huku tathmini ikiendelea, na mvua zaidi inatarajiwa katika siku zijazo.
Raia wametakiwa kuondoka kutoka kwenye maeneo ya mito yaliyo hatarini kukumbwa na mafuriko. Afghanistan inaendelea kukabiliwa na majanga ya hali mbaya ya hewa yanayochangiwa na mabadiliko ya tabianchi.