1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu wanane wafariki katika mkanyagano AFCON

25 Januari 2022

Watu wanane wamefariki dunia siku ya Jumatatu, katika tukio la mkanyagano nje ya uwanja ambako Cameroon ilikuwa inacheza dhidi ya Comoro, katika mechi ya kufuzu robo fainali ambayo Cameroon imeshinda kwa magoli 2-1.

Fußball Africa Cup of Nations
Picha: MOHAMED ABD EL GHANY/REUTERS

Wenyeji wa michuano hiyo Cameroon wameweka miadi ya robo fainali dhidi ya Gambia, baada ya kupambana kushinda magoli 2-1 dhidi ya Comoro, katika mechi iliyoshuhudia vifo vya watu wasiopungua wanane na dazeni kadhaa wengine wakijeruhiwa katika mgandamizo nje ya uwanja wa Olembe mjini Yaounde, ambako mechi hiyo ilichezwa.

Gavana wa mkoa wa Kati wa Cameroon, Naseri Paul Biya, amesema huenda kukawa na vifo zaidi. Maafisa katika hospitali ya karibu ya Massassi wamesema wamepokea majeruhi wasiopungua 40, waiokimbizwa hospitali hapo na polisi na raia. Maafisa hao wamesema hospitali hiyo haikuwa na uwezo wa kuwatibu.

Soma zaidi: Cameroon yaizima Comoro AFCON, Gambia yatinga robo fainali

Mashuhudua waliokuwepo uwanjani wamesema watoto walikuwa miongoni mwa waliokumbwa na mkasa, ambao ulitokea baada ya wasimamizi wa uwanja kufunga milango na kusitisha kuwaruhusu watu kuingia. Maafisa wa soka wamsema karibu watu 50,000 walijaribu kuhudhuria mechi hiyo.

Picha: DANIEL BELOUMOU OLOMO/AFP/Getty Images

Uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamanaji 60,000 lakini haukupaswa kuja kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona. Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, linaloendesha michuano ya kombe la Afrika, limesema linafahamu juu ya tukio hilo.

Mmoja ya maafisa wa juu wa shirikisho hilo, katibu mkuu Veron Mosengo-Omba, alikwenda kuwatembelea mashabiki waliojeruhiwa hospitalini, imesema CAF katika taarifa na kuongeza kuwa inafanya uchunguzi kubaini hasa chanzo cha mkanyagano huo.

Soma pia: Algeria yashindwa kulitetea taji lake AFCON

Wasiwasi juu ya utayarifu wa Cameroon

Cameroon inaandaa kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 50. Ilipaswa kuandaa mashindano hayo mwaka 2019 lakini ilinyanganywa fursa hiyo na kupewa Misri, kutokana na wasiwasi mkubwa juu ya maandalizi ya Cameroon, hasa utayarifu wa viwanja vyake.

Samuel Eto'o atafuta sifa ndani na nje ya uwanja

01:29

This browser does not support the video element.

Uwanja wa Olembe ulikuwa moja ya viwanja vilivyokuwa chini ya ucunguzi, na ndiyo uwanja mkuu wa mashindano hayo ya mwezi mzima, na unatarajiwa kutumika kwa mechi nyingine tatu, ikiwemo fainali hapo Februari 6.

Soma pia: 

Tukio la jana ndiyo la pigo kubwa la pili kwa taifa hilo katika muda wa siku moja, baada ya watu 17 kufariki kutokana moto uliosabishwa na mkururo wa milipuko kwenye klabu ya usiku siku ya Jumapili.

Soma pia: Iheanacho awafunika Salah, Mahrez katika AFCON

Kufuatia tukio hilo, rais wa Cameroon Paul Biya ameihimiza nchi kuwa katika tahadhari wakati ikiwa mwenyeji wa tukio kubwa zaidi la kimichezo katika nusu karne.

Cameroon imeshinda mchezo wa jana kwa magoli 2-1 na kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali, ambapo itacheza dhidi ya Gambia siku ya Jumamosi.

Wachezaji wa Gambia wakisherehekea bao lao ambalo ndiyo lilikuwa na ushindi dhidi ya Guinea.Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Gambia iliishinda Guinea katika mechi iliyochezwa awali kwa kuifunga goli 1-0, ambalo lilitiwa kimyani na fowadi Musa Barrow katika dakika 71.

Ingawa Guinea iko nafasi 69 juu ya Gambia katika orodha ya timu bora za dunia, hakukuwa na cha kuchagua kati ya pande mbili, baada ya nusu ya kwanza katika uwanja wa Bafoussam, magharibi mwa Cameroon.

Hatua ya 16 bora itaendelea Jumanne hii ambapo Senegal itacheza na Cape Verde mjini Bafoussam kabla ya Morocco kumenyana na Malawi mjini Yaounde.

Chanzo: Mashirika