1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroPakistan

Watu wanane wauawa katika shambulizi Pakistan

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Maafisa wa usalama wamesema mshambuliaji alianzisha mlipuko huo kutoka pikipiki karibu na mji wa Mir Ali katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa.

Watu wanane wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga magharibi mwa Pakistan
Watu wanane wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga magharibi mwa PakistanPicha: Mehboob Ul Haq/AFP/Getty Images

Maafisa wanne wa polisi waliuawa pamoja na wasaidizi wawili wa jeshi na raia wawili katika shambulio karibu na mpaka na Afghanistan.

Taarifa ya polisi imesema watatu miongoni mwa watao waliojeruhiwa wako katika hali mbaya. Shambulio hilo lilidaiwa na kundi la wanamgambo wasiojulikana wanaojiita "Aswad ul-Harb".

Pakistan imeshuhudia ongezeko la wanamgambo tangu kundi la Taliban la Afghanistan kurejea madarakani mwaka 2021, huku Islamabad ikidai makundi hasimu sasa yanatumia nchi hiyo jirani kwa hifadhi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW