1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Watu wanane wauawa Odessa kufuatia mashambulizi ya Urusi

20 Desemba 2025

Takriban watu wanane wameuawa na wengine 27 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kombora la Urusi usiku wa kuamkia leo katika mji wa bandari wa Odessa nchini Ukraine.

Odessa | Jengo la ghorofa likiteketea kwa moto kufuatia shambulio la Urusi
Jengo la ghorofa likiteketea kwa moto kufuatia shambulio la Urusi huko Odessa.Picha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Basi la abiria lililengwa huku malori yakiwaka moto katika eneo la maegesho ya magari. Taarifa hiyo iliyotolewa na Huduma ya Ulinzi wa Raia ya Ukraine haikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru vya habari. Pia, jeshi la Ukraine limesema limeshambulia kwa droni na kuharibu kituo cha kuchimba mafuta cha "Lukoil" pamoja na meli ya kivita ya Urusi ya "Ochotnik" katika Bahari ya Caspian, takriban kilometa 1,800 kutoka pwani ya Ukraine.

Hayo yakiarifiwa, Mjumbe wa Urusi Kirill Dmitriev amesema hivi leo kuwa anaelekea katika mji wa Miami ambako duru nyingine ya mazungumzo ya kujaribu kuutatua mzozo wa Ukraine imepangwa kufanyika. Marekani imekuwa ikijaribu kwa muda sasa kuutafutia suluhu  mzozo huo  uliodumu kwa karibu miaka minne.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW