1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wafa katika ajali ya moto huko Bukavu

10 Juni 2024

Watu 4 wamefariki katika ajali ya moto iliyotekeza pia mali usiku wa kuamkia Jumatatu hii huko mjini Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Afrika, Bukavu
Miongoni mwa maeneo za Bukavu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kumekuwepo na ajali za moto kwenye reneo hilo zinazoibua kitisho kwa wakaziPicha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Kiongozi wa mtaa wa Kadutu ulikotokea moto huo, Jan Mizinzi Murhandikire, amethibitisha tukio hilo ingawa chanzo bado hakijafahamika.

Ajali nyingine ya moto imeteketeza nyumba 29 usiku wa kuamkia leo Jumatatu katika mtaa huo huo wa Kadutu eneo la Nyamungo.

Mizinzi amesema ajali zote zilitokea katika maeneo ambayo magari ya zimamoto yasingeweza kufika kwani nyumba zilizojengwa zimebana njia. 

Aidha kiongozi huyo alidokeza juu ya mkutano wa dharura unaofanyika Jumatatu hii mjini Bukavu ili kuweka mikakati kambambe ya kukabiliana na ajali za moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW