Asili na mazingiraMarekani
Watu wanne wafariki dunia kutokana na vimbunga, Oklahoma
29 Aprili 2024Matangazo
Vimbunga hivyo vilisababisha uharibifu mkubwa katika mji wa Sulphur, ulio na idadi ya takriban watu 5,000 ambapo vimbunga hivyo vilisababisha kuporomoka kwa majengo, kupindua magari na kubomoa paa za nyumba.
Biashara zaathirika kutokana na vimbunga
Wakati wa ziara katika mji huo wa Sulphur, Gavana wa jimbo hilo la Oklahoma Kevin Stitt alisema kwa jinsi inavyoonekana, kila biashara mjini humo iliharibiwa.
Soma pia:Kimbunga chauwa zaidi ya watu 70 Marekani
Maafisa wa ikulu ya White House wamesema kuwa Rais wa nchi hiyo Joe Biden alizungumza na Stitt jana na kutoa msaada kamili wa serikali hiyo ya shirikisho.