1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wafariki kufuatia mafuriko kusini mwa Ujerumani

4 Juni 2024

Mafuriko yanayoshuhudiwa kusini mwa Ujerumani yamesababisha vifo vya watu wanne huku maelfu ya wengine wakilazimika kuondoka kwenye makazi yao.

Maji yaliozingira makaazi ya watu.
Maji yakifunika barabara na kuingia mitaani kwenye makaazi ya watu katika moja ya mitaa kwenye jimbo la BavariaPicha: ANNA SZILAGYI/EPA

 

Mvua kubwa zilianza kunyesha siku ya Ijumaa kwenye majimbo ya Bavaria na Baden Wuerttenberg na hivyo mito eneo hilo kuongezeka ujazo wake na kupelekea mafuriko makubwa. Afisa mmoja wa kikosi cha uokoaji amesema maji yamejaa katika maeneo mengi. 

"Eneo hili kiwango cha maji kipo chini, lakini huko kwengineko, kuna mafuriko makubwa na maeneo mengine yamejaa maji hadi kwenye ghorofa ya kwanza ya majumba. Hakika hili ni janga."

Soma pia:Juhudi za kuwahamisha waliokumbwa na mafuriko Ujerumani zaendelea

Takwimu za mamlaka ya Hali ya Hewa ya Ujerumani (DWD) zinaonesha kuwa mafuriko haya yasiyo ya kawaida hutokea mara moja tu kila baada ya miaka 50 au 100.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW