1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wajeruhiwa katika vurugu za mechi mjini Tunis

12 Mei 2022

Watu wanne wamejeruhiwa huku mmoja akiwa hali mahututi katika vurugu za mashabiki hasimu, zilizozuka kwenye mchezo wa fainali wa kombe la mpira wa mikono nchini Tunisia.

Tokio 2020 | Handball Herren | Portugal vs Ägypten
Picha: REUTERS

Mechi hiyo ilikuwa baina ya timu mbili pinzani za mji mkuu wa Tunis za Esperance na the African Club.

Msemaji wa huduma ya dharura amesema watu hao wamelazwa hospitali kutokana na majeraha ya moto baada ya mashabiki wa timu hizo mbili hasimu kurushiana vilipuzi katika uwanja wa michezo wa Rades.

Mikanda ya video ya mechi hiyo imeonyesha kile kilichooonekana kuwa ni moto wa fashifashi zilizowashwa na upande wa uwanja uliofurika mashabiki.

Waamuzi walilazimika kusimamisha mechi katika dakika ya 10 na polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuondoa watu uwanjani.

Mechi hiyo imeahirishwa na mashabiki wa timu hizo mbili watakabiliwa na adhabu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW