1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wauawa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine

14 Novemba 2025

Urusi imefanya shambulizi la takriban droni 430 pamoja na makombora katika safu mpya ya mashambulizi mabaya ya usiku kucha dhidi ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu wa Kiev.

Urusi -Kursk- 2025 | shambulizi la Ukraine
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la Ukraine nchini Urusi mnamo Januari 2, 2025Picha: REUTERS

Kulingana na msimamizi wa jeshi mjini Kiev, Tymur Tkachenko, takriban watu wanne waliuawa na wengine 27 kujeruhiwa katika tukio hilo. Majeruhi 15 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.

Zelensky asema shambulizi la Urusi Kiev ni la kushtukiza

Katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelitaja shambulizi hilo kuwa la ''kushtukiza'' lililolenga miundombinu ya kiraia na akachapisha picha na video zinazoonyesha nyumba zilizoharibiwa vibaya.

Ubalozi wa Azerbaijan mjini Kiev pia ulilengwa na kuharibiwa na vipande vya makombora.

Kulingana na Zelensky, Kiev ndio ilikuwa shabaha la mashambulizi hayo, lakini maeneo ya karibu pamoja na yale ya Kharkiv na Odessa pia yaliathirika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW