1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wauawa kufuatia mashambulizi ya roketi huko Lviv

6 Julai 2023

Watu wanne wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa kufuatia shambulio la roketi usiku wa kuamkia leo kwenye eneo la makaazi katika mji wa magharibi mwa Ukraine wa Lviv.

Raketenangriff Lviv Lwiw Ukraine
Picha: STATE EMERGENCY SERVICE OF UKRAINE/REUTERS

Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya ndani ya Ukraine na kubaini kuwa shughuli ya uokoaji bado inaendelea.

Zaidi ya watu saba wameokolewa kutoka kwenye vifusi huku wengine 60 wakihamishwa kutokana na nyumba zao kuharibiwa.

Meya wa Lviv, Andriy Sadovyi, amesema ni shambulio baya zaidi dhidi ya miundombinu ya raia wa Lviv tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi ambapo zaidi ya nyumba 50 zimeharibiwa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram kuwa bila shaka kitendo hicho alichokiita "shambulio la magaidi wa Urusi" kitajibiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW