1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Watu wanne wazuiliwa na polisi kwa kuwatembeza wanawake uchi

21 Julai 2023

Polisi nchini India inawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuwatembeza wanawake wawili wakiwa uchi mbele ya kundi la watu.

Symbolbild Polizist in Maharashtra
Picha: INDRANIL MUKHERJEE/AFP

Washukiwa hao walitambuliwa baada ya kipande cha video cha tukio hilo lililotokea mapema mwezi Mei katika jimbo la Manipur, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua ghadhabu kote nchini India.

Kwenye video hiyo, wanawake hao walionekana wakitembea kando ya barabara wakiwa uchi huku wakidhihakiwa na kundi la watu. 

Soma piaHaswa baina ya madhehebu ya Wahindu na Waislamu

Waziri kiongozi wa serikali ya jimbo hilo la Manipur, lililokumbwa na ghasia za kikabila Biren Singh, amesema kupitia Twitter kwamba tayari polisi wanachunguza kisa hicho.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi, anayekabiliwa na ukosoaji kutoka upinzani, hapo jana amezungumzia kisa hicho kwa mara ya kwanza hadharani, akisema kimeliaibisha taifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW