1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBangladesh

Watu wapatao 15 wauwawa kwenye ajali ya treni Bangladesh

24 Oktoba 2023

Ajali hiyo ilitokea wakati mabehewa mawili ya nyuma ya treni ya abiria iliyokuwa njiani kuelekea Dhaka yalipogongwa na treni ya mizigo.

Watu wapatao 15 wauwawa kwenye ajali ya treni Bangladesh
Watu wapatao 15 wauwawa kwenye ajali ya treni BangladeshPicha: Bangladesh Fire Service and Civil Defense Department/AP Photo/picture alliance

Treni ya mizigo imeigonga treni ya abiria nje ya mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka jana Jumatatu na kusababisha vifo vya watu wapatao 15 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea wakati mabehewa mawili ya nyuma ya treni ya abiria iliyokuwa njiani kuelekea Dhaka yalipogongwa na treni ya mizigo iliyokuwa ikielekea Chattogram.

Afisa wa zima moto Mosharraf Hossain amesema waokoaji walijumuika na wakazi katika juhudi za kuwatoa abiria kutoka kwa mabaki ya mabehewa huko Bhairab katika wilaya ya kati ya Kishoreganj, ambako ajali hiyo ilitokea.

Amesema miili ya watu wapatao 15 imeopolewa na idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Haikubainika ni watu wangapi ambao wamenasa ndani ya mabaki ya treni hizo. Haikufahamika mara moja kitu kilichosababisha ajali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW