1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu wasiopungua 18 wauawa katika maporomoko ya taka Uganda

12 Agosti 2024

Dampo kubwa la taka limeporomoka katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, na kusababisha vifo vya watu wasopungua 18 na kuwajeruhi wengine 14.

Maporomoko ya dampo la taka Uganda
Waokoaji wakitoa maiti kwenye vifusi vya mapromoko ya taka KampalaPicha: Simon Tumwine/XinHua/dpa/picture alliance

Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, KCCA, imesema katika taarifa kwamba waathirika wasiopungua wawili kati ya waliokufa katika maporoko hayo ya dampo la Kiteezi ni watoto.

Maporomoko ya dampo hilo, ambalo linahudumia sehemu kubwa zaidi ya mji wa Kampala, yanaaminika kusababishwa na mvua kubwa.

Haijabainika wazi kuhusu kilichotolea hasa, lakini mamlaka za jiji zilisema dampo hilo lilishindwa kuhimili uzito wa taka.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo, akihoji katika machapicho kadhaa kwenye mtandao wa kijamii wa X, kwanini watu walikuwa wanaishi karibu na rundo la taka lisilo salaama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW